Kitabı oku: «Kuelezea Ni Nani Barack Obama Kikamilifu»
Kuelezea Barack Obama Kikamilifu
Jina La Mwandishi: Celine Claire
Jina La Mtafsiri: Ephraim Kamau Njoroge
© Haki Miliki – Haki zote zimehifadhiwa.
Sio halali kuzalishana, kunakili au kusambaza sehemu yoyote ya kitabu hiki kwa njia ya electroniki, mtandao au kwa uchapaji kwa makaratasi. Kurekodi uchapishaji huu ni marufuku kabisa na uhifadhi wowote wa kitabu hiki hairuhusiwi isipokuwa kwa idhini iliyoandikwa kutoka kwa mchapishaji, isipokuwa matumizi ya nukuu fupi katika hakiki ya kitabu.
Barack Obama ni nani?
Barrack Hussein Obama alizaliwa tarehe 4th Agosti 1961 kule Honolulu, Hawaii. Yeye ni mwana siasa wa Marekani na pia mwana sheria aliyehudumu kama Rais wa Arobaini na Nne (44) Marekani kwa mihula miwili katikati ya 2009 na 2017. Mzazi wake mmoja alitoka nchi ya Kenya na mwingine alitoka Kansas, Marekani. Babake Barrack Obama, Barrack Obama Senior, ni wa uzao wa jamii ya Waluo kutoka mkoa wa Nyanza, katika nchi ya Kenya.
Babake Obama alifanya kazi ya kuchunga mbuzi katika bara la Afrika. Hatimaye, alipata udhamini uliomruhusu kutoka Kenya na kufuatilia ndoto yake ya kuendelesha masomo yake kwa chuo kikuu mle Kansas. Wakati wa Vita ya Pili ya Ulimengu, mamaye Obama, Ann Dunham, alizaliwa katika Kituo cha Jeshi cha Wichita, Kansas.
Babake Obama alipokuwa akifuatilia masomo yake pale chuoni ya Hawaii, Manoa, alikutana na mwanafunzi mwenzake, Ann Dunham. Hawa wawili walipata kuoana mnamo tarehe 2ndFebruari 1961, naye Obama Junior akazaliwa miezi sita baadaye. Obama Senior aliondoka punde tu baada ya Obama Junior kuzaliwa, na pia wao wawili wakatalakiana miaka miwili baadaye. Mwakani wa 1965, Ann Dunham aliolewa tena kwa Lolo Soetoro, mwanafunzi wa chuo kikuu cha Hawaii, kutoka Indonesia.
Miezi kumi na miwili baadaye, jamii hii changa ikahamia Jakarta, Indonesia, pahali ambapo dadake-wa-kambo Obama Junior, Maya Soetoro Ng alizaliwa, mwakani wa 1970. Matukio kadhaa mle Indonesia ilimuacha Ann Dunham na mashaka juu ya usalama na masomo ya Obama Junior. Kwa hivyo, alipokuwa na umri wa miaka kumi, Obama Junior alirejeshwa mle Hawaii kuishi na wazazi wa mama yake. Baadaye, Ann Dunham na dada yake wa kambo, Maya Soetoro Ng, wakajiunga na wao.
Kukua Kwake Barack Obama Junior
Alipokuwa akikua kama mtoto, Barack Obama Junior hakuwa na uhusiano na baba yake. Baado Obama Junior akiwa mtoto mchanga, babake alihamia Massachusetts kufuatilia shahada ya Ph.D mle chuoni ya Harvard. Wazazi wa Obama Junior walitengana kirasmi baada ya muuda na hatimaye kutalakiana mwezi wa Machi 1964, wakati ambapo Obama Junior alikuwa na miaka miwili. Baada ya muda kidogo, Obama Senior akarejea Kenya.
Barack Obama aliendelea kung’ang’ana na maisha bila baba yake utotoni wake, ambaye alimuona safari moja tu baada ya wazazi wake kutalakiana. Hii ilikuwa wakati Obama Senior alitembea Hawaii kwa muda mfupi mnamo 1971.”
[Babangu] alikuwa ameacha paradiso, na hakuna jambo lolote ambalo mama au babu zangu wangeniambia lingeondoa ukweli huu pekee usioweza kupingwa,” Obama Junior akaangazia baadaye. “Hawangeweza kuelezea jinsi mambo ingekuwa kama baba angekuweko.”
Alipokuwa akiishi na wazazi wa mama yake, Obama Junior alijisajili kwenye chuo kinachoheshimiwa cha Punahou. Huko akafaulu sana katika Mchezo wa Kikapu na kufuzu kwa hali ya juu katika taaluma yake, mwakani wa 1979. Kwa maana alikuwa mmoja kati ya wanafunzi watatu pekee Weusi kwa chuo hicho, Obama Junior alikuja kufahamu maana ya ubaguzi wa rangi na maana hakika ya kuwa Mu-Marekani wa asili ya Ki-Afrika.
Obama Junior baadaye alielezea vile alishumbuka kupatanisha mitazamo ya kijamii ya uridhi wake wa kimataifa na hisia zake za ubinafsi. Nikafahamu ya kwamba hapakuwa na yeyote kama mimi kwenye orodha ya bidhaa za Christmasi ya Sears - Roebuck, na pia Santa alikuwa mtu mweupe.
Obama Junior akaandika, “Nilienda kwenye bafu na kusimama mbele ya kioo kwa ufahamu wangu wote na miguu ikiwa imara, nikitazama kama nilikuwa nafanya hapo awali, na nikashangaa kama palikuwa na kitu mbaya ndani yangu.
Obama alihudhulia shule wapi?
Barack Obama alijiunga na chuo cha Occidental kule Los Angeles mwakani wa 1979. Baada ya miaka miwili, Barack Obama akahamia chuo kikuu cha Columbia kule New York na akahitimu mnano mwaka wa 1983 na shahada ya Sayansi ya Kisiasa. Barack Obama alihitimu kutoka chuo kikuu cha Havard kwa kiwango cha kuheshimika cha Magna cum laude.
Baada ya kuhitimu chuoni kikuu cha Columbia kwa Shahada ya Kwanza, Barack Obama Junior alifanya kazi kwa miaka miwili katika Tasnia ya Biashara. Kisha akahamia Chicago mwakani wa 1985, pahali alifanya kazi kusini mwa jimbo hiyo ambayo ni duni, akihudumu kama mratibu wa wakaazi wa mapato ya chini, pale Roseland na Jamii za Altgeld Gardens
Kwa wakati huu, Obama Junior alisema ya kwamba “hakulelewa kwenye boma yenye udini.” Huu ndio pia wakati alijiunga na Kanisa la Muungano wa Utatu wa Kristo, yaani Trinity United Church of Christ. Akawatembelea jamaa zake kwenye nchi ya Kenya. Akaenda kuangalia kaburi ya babake mzazi, Barack Obama Senior, aliyefariki kwenye ajali ya gari mwezini wa November 1982, na pia kaburi ya baba wa baba yake.
Obama Junior akaandika: “Kwa muda mrefu niliketi katikati ya kaburi hizi mbili na kulia. Nikaona ya kwamba, maisha yangu Marekani – maisha ya uWeusi, maisha ya uweupe, hisia ya kuachiliwa ambayo niliihisi nikiwa mvulana, kufadhaika na tumaini niliyoshuhudia kule Chicago – hii yote ilikuwa na uhusiano na sehemu hii ndogo ya ardhi iliyokuwa umbali wa kuvuka bahari.
Akirejea kutoka Kenya akiwa na hisia ya kufanyiwa upya, Barack Obama aliingia Shule ya Sheria ya Havard mwakani wa 1988. Mwaka uliofuata, Obama akakutana na Profesa wa sheria ya katiba, Laurence Tribe. Wakafanya mazungumzo iliyomvutia profesa. Wakati Barack Obama aliomba kujiunga na timu ya Professor kama mtafiti msaidizi, alikubaliwa.
Profesa Laurence Tribe alisema mwakani wa 2012 katika mahojiano na Frontline, “Alivyofanya bora zaidi kule Shuleni ya Sheria ya Havard, na zaidi alivyovutia watu, zaidi ndivyo ilikuwa wazi ya kwamba angefikia chochote. Lakini ilikuwa wazi ya kwamba haja yake ilikuwa kuleta utofauti kwa watu, kwa jamii
Mwakani wa 1989, Barack Obama alijiunga na Sidley Austin, Kampuni ya Sheria ya Chicago, akiwa mshirika mwenza wakati wa muhula wa joto, ambapo alikutana na mke wake wa sasa, Michelle Obama. Mwezini wa Februari 1990, Barack Obama alichaguliwa kama Mhariri wa “Havard Law Review” wa kwanza Mu-Marekani wa asili ya Ki-Afrika.
Doa yake na Michelle Obama na wasichana wake
Barack Obama Junior alikutana na Michelle Robinson, mwana sheria kijana aliyepewa jukumu kama mshauri wake kwenye kampuni ya sheria ya Sidley Austin kule Chicago. Baadaye, hawa wawili walianza kuchumbiana, na mnamo 3rd Oktoba 1992, Barack Obama na Michelle walikuwa kwenye ndoa yenye furaha.
Ücretsiz ön izlemeyi tamamladınız.